Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TIMU ya soka ya Kisiju Fc inayotokea Kata ya Kisiju imekuwa ya kwanza kutangulia hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Mbunge Ulega (Ulega Jimbo Cup) baada ya kuifunga timu ngumu  ya Lukanga Fc kwa bao 1-0.
Kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Mkuranga ambao pia ulihudhuliwa na wanhanchi wengi pamoja na mbunge  Abdallah Ulega, timu zote zilionesha uwezo mkubwa wa kucheza soka la uhakika huku maelfu ya watazamaji waliohudhulia. 
 Waamuzi mchezo huo iliyochezeshwa jana ni, Niacheni Mohamed aliyesaidiwa Mtuwi Stanley  pamoja na Mharami Mahenga.Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji ambayo yaliinufaisha timu ya Kisiju ambayo ilijipatia bao la pekee katika  dakika ya 62 lililofungwa na Mud Mbwete aliyeunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na mchezaji Mohamed Taita iliyounganishwa na Mbwete na kujaa wavuni.
Baada ya bao hilo Lukanga waliongeza kasi ya mashambulizi wakitaka kupata bao la kusawazisha lakiki walinzi wa Kisiju na kipa wao Hassani walikuwa imara. 
Timu  ya kisiju inaingia fainali ya Ulega Cup itakayofanyika mwanzoni mwa machi mwaka huu
Akizungumzia mchezo hio  Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega aliwashukuru waamuzi kwa kuchezesha kwa umakini sanjali na wachezaji wa timu zote mbili kwa kuonesha mchezo wenye nidhamu na kuongeza  kuwa vijana wameonesha uwezo  katika kucheza soka.
 Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na wachezaji katika mchezo wa Nusu Fainali  kati ya timu ya  ya kisiju na Lukanga katika kiwanja mpira Mkuranga.
 Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na timu ya Kisiju FC
 Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na timu ya Lukanga FC
 Mchezo ukiendelea kati ya uwanja
Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Nusu fainali katika ya timu ya  ya Kisiju na Lukanga katika kiwanja mpira Mkuranga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi sana....Wana Mkuranga tuendeleze sana michezo... maxsportstz.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. www.maxsportstz.blogspot.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...