Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wasanii na vikundi vinavyopiga muziki wa bendi wametakiwa kujitazama upya juu ya muziki huo kutumika kama chombo cha kuuzia bia kwenye Bar.
Hayo yamesemwa na msanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini John Kitime alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habri katika jukwaa la sanaa liliandaliwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA).
“Kuna vitu tunafanya tunaona kama vya kawaida lakini ndio vinaua muziki wetu kama leo hii bendi zinapiga kwenye bara kwa ajili ya kuuza bia na watu wanaangalia bure hivyo inamaanisha bendi zetu ndio kichocheo cha kuuza pombe katika mabaa yote mjini”amesema Kitime.
Kitime ametoa wito kwa wasanii kuanza kubadilisha mtindo wa maisha kwani kitendo cha bendi zote kuhamia kwenye bar ni moja ya anguko kubwa la muziki wa dansi nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...