Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi.
Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.
Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.
Pia mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.
“Katika kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam. 
 Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...