Familia ya Marehemu Mh. Samuel Sitta inawatangazia ndugu, jamaa, majirani na marafiki kuwa imepata pigo la kuondokewa na Mdogo wa Marehemu Mhe. Samuel Sitta, ambaye alikuwa Meya wa mji mdogo wa Urambo Ndg. Peter Sitta.
Marehemu Peter Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamos katika hospital ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam. Msiba upo Masaki nyumbani kwa Hayati Samuel Sitta Mtaa wa Twiga Karibu na Makao makuu ya UNHCR jijini Dar es salaam.
Bwana ametoa,
Bwana ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe.
AMEN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...