NG’OMBE waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamatarjiwa kupigwa mnada kufuatia uamuzi wa mahakama.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati alipokwenda kukagua lindo la ng’ombe hao, jana eneo la Mgagao, wilayani Mwanga, walikohifadhiwa.

“Kufuatia uamuzi wa mahakama, ng’ombe hawa watauzwa kwa njia ya mnada siku ya Ijumaa, Oktoba 20, mwaka huu, kutokana na hali za ng’ombe hawa kutokuwa nzuri”, alisema.
Aliongeza, “Tayari mahakama imeridhia ombi la serikali la kutoka kuuzwa kwa ng’mbe hawa na ishamteua dalali wa kufanya mnada huo ambaye ni Marepelanto ya mjini Moshi na kazi hii itafanywa haraka kutokana na ng’ombe wengine kuanza kufa, kama mlivyosikia tayari sita wameshakufa”.

Aidha alisema serikali itaanza operesheni maalum ya kuwakamata ng’ombe walioingizwa nchini kinyume cha sehria kuanzia Jumatatu ijayo.

“Baada ya operesheni ya hapa Kilimanjaro, nilitoa siku saba kwa Mikoa mingine kuiondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria kupitia Mikoa hiyo, muda huo umekwisha, Jumatatu tunaanza ingine itakayochukua siku 15 ili kuhakikisha mifugo hiyo inaondolewa yote”, alisema.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katikati, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Aaron Mbogho, kushoto kwake katibu tawala wa wilaya ya Mwanga Bw. Yusuph Kasuka wakiangalia ng'ombe waliotaifishwa wakati wakinywa maji katika kijiji cha Mgagau wilayani Mwanga.
Waziri Mpina , Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Maria Mashingo na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aaron Mbogho wakijadili jambo baada ya kuongea na wanahabari kuhusu amri ya mahakama ya kupiga mnada ngombe walitaifishwa na Serikali.
Ng’ombe walioamriwa na mahakama kupigwa mnada, mnada utapigwa siku ya ijumaa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...