Vijana nchini wametakiwa kujiajiri kupitia kilimo badala ya kukimbilia nchi za nje kama njia ya mkato ya kutafuta maisha. Wito huo umetolewa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati akiyafunga rasmi maonesho ya siku ya chakula duniani yaliyofanyika kitaifa huko Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A.

Amesema ni aibu kuona vijana wengi wa Kiafrika wanapoteza maisha baharini Mediterrania kwa safari za kwenda ulaya kutafuta maisha wakati Bara la Afrika lina fulsa nyingi za ajiri kupitia sekta ya kilimo. Akizunzungumzia kuhusu mikopo kwa wakulima wadogo wadogo Balozi Seif amezitaka taasisi za fedha nchini kutoa mikopo nafuu kwa wakulima hao kama hatua ya kuiunga mkono serikali ya kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini.

Amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuazisha viwanda vidogo vidogo vinavyotumia mali ghafi ya kilimo kutoka hapa nchini jambo ambalo litawasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa wingi na kujiongezea kipato chao.

Kuhusu maonesho Makamo wa Pili wa Rais ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea wananchi wengi wa Zanzibar kuhudhuria maonesho hayo. Amesema Serikali imejipanga kuyafanya maonesho ya kilimo hapa nchini kuwa endelevu na kuzitaka taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya Kilimo kuliendeleza eneo hilo la Kizimbani kwa kuweka miundo mbinu ya kudumu. 

Wakati huo huo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametowa zawadi ya kikombe kwa Jeshi la Kujenga Uchumi kwa kuwa mshindi wa Kwanza wa maonesho ya siku ya chakula duniani mwaka huu hapa Zanzibar.

Kutokana na ombi la wananchi wengi maonesho hayo ya kilimo yataendelea kwa siku moja zaidi ili kutoa nafasi kwa wananchi kufaidika na taaluma ya kilimo inayotolewa pamoja na kununua bidhaa mbali mbali za kilimo.

Aidha Serikali imekusudia kutoa fursa kwa wakulima kuuza bidhaa zao kila wiki katika eneo hilo la maonesho ili kutoa fursa kwa wakulima kuwapatia soko la uhakika.
Balozi Seif akiangalia zana za kilimo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza ununuaji wa zana za kisasa za kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Balozi Seif akipata maelezo kuhusu ufugaji wa mbuzi wa kisasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...