Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui. Tuzo hiyo  ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo. 

Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita. Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini.
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti cha Tuzo hiyo Dkt. Salim
Balozi Chergui akimkabidhi Tuzo ya Juu  ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika ya Mwaka 2014, Binti wa Balozi Hashim Mbita, Sheila Hashima Mbita ambaye aliipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Baba yake ambaye hakuweza kufika kutokana na matatizo ya kiafya.
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti Bi. Sheila Hashim Mbita kwa niaba ya Balozi Mbita. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Hashim Mbita, nakupa pole nasikia una matatizo ya afya. Naomba kuwa yawe matatizo madogo. Naandika kukupa mkono na kukucongratulate kwa tunukio hili. Nakukumbuka sana tulikuwa pamoja enzi za Mr Blummer Tabora school. Miye nilikuwa Tembo nawe Kiboko. Congratulations.God bless.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...