Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, kwa
pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa
Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo
Julai 3,2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, Wilayani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,
leo.
Baadhi ya wawakilishi wa makampuni na Mashirika waliohudhuria hafla hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipata maelezo kuhusu ramani ya Jengo hilo la TTCL, kutoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya 'Quality Buildin Contractors Ltd',
Khamis Ally Shaibu, wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi
katika Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, iliyofanyika leo Wilayani
Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...