Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico),Zena Kangoyi
akizungumza na waandishi wa habari juu mafanikio ya stamico baada ya maboresho
yaliyofanywa katika shirika hilo katika Ofisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa
Utafiti na Uchorongaji ,Alex
Rutagwelela akizungumza na waandishi wa habari juu Stamico linavyosimamia
majukumu yake katika katika kuendeleza wachuimbaji wadogo iliyofanyika leo
Makao Makuu ya Stamico,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala,Beatrice akizungumza na waandishi wa habari juu Stamico
linavyoweza kusimamia miradi yake na uwezo wa Shirika hili iliyofanyika leo
Makao Makuu ya Stamico jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico,Zena Kangoyi
akiwa na baadhi ya wakurugenzi wakati akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa
waandishi wa habari iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico)limesema kuwa
kutokana na kuwepo kwa maboresho katika shirika hilo limezidi kujitanua katika
utoaji wa utaalam kwa wachimbaji wadogo jinsi ya kuchimba madini kisasa na
kuachana uchimbaji duni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,Zena Kongoyi amesema kuwa shirika licha ya
kuweka miradi ya kusaidia wachimbaji wadogo lakini wameweza kuwekeza uchimbaji
wa madini kwa kushirikiana na kampuni zingine kutokana sharia ziliwekwa baada ya
mabaoresho ya shirika hilo.
Amesema baadhi ya miradi ya uzalishaji wa madini
imeanza kuzalisha na kuweza shirika kutoka hatua moja kwenda nyingine katika katika utaoji huduma pamoja
kukuza uchumi wa nchi pamoja kuongeza ajira nchini kutokana na miradi ya
uzalishaji wa dhahabu.
Zena amesema kuwa shirika limeanzisha miradi
kuendeleza wachimbaji wadogo kitaalamu na ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya
Nishati na Madini pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu (SMMRP) katika
kuwaondoa katika uduni.
Amesema katika mradi wa Stamigold umesafirisha na
kuuza dhahabu katika nchi ya Switzerland kwa kiasi cha Wakia 12,923.35 na
kuingizia shirika la Taifa la Madini (Stamico)na taifa kwa ujumla Dola za
Kimarekani Milioni 15.6. na kuaza kurejesha mrabaha wa asilimia 4.0 ya mauzo
sawa n ash.1.3 za serikali na Wizara ya Nishati na Madini na kulipa ushuru
sh.milioni 40..
Aidha amesema shirika limeweza kuanzisha mradi wa
ununuzi wa madini ghafi ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya
vijiji vya Kabingo,Murongo ,Syndicate na Rugasha katika Wilaya Kyerw,mkoani
Kagera na kuyauza madini hayo kwenye
soko la nje ya nchi ikiwa na lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo .
Zena amesema wako katika mazungumzo na Benki ya TIB kuweza
kukopa Dola za Kimarekani 700,00090000
kwa ajili ya kununua mitambo hali ambayo shirika litaweza kukua katika
kuendesha miradi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...