Mpira umeanza kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo Serengeti Boys wanaonekana kutawala mpira na katika dakika ya 15 Nickson Kibabage anaiandikia Serengeti goli la kwanza akitumia maridadi mguu wake kushoto na kutinga nyavuni.

Dakika ya 22, Ibrahim Ally anaiandikia Stars goli la pili ikiwa ni shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.Mpira umeonekana kuchezwa upande mmoja na Serengeti kukosa nafasi nyingi za wazi.Mpira ni mapumziko na Serengeti wanatoka wakiwa mbele kwa goli 2.

Kipindi cha pil kimeanza na timu zote kuwa makini ambapo dakika ya 60, Ally Msengi anaiandikia Serengeti goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Shelisheli kuushika ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru penati.
   
Mchezo kati ya Serengeti Boys na Sechelles unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0. 
 Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakishangilia mara baada ya kupata goli. 
Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Rashid Mohamed Chambo akimchomoka mchezaji wa timu ya Sechelles,katika mchezo wao unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza  bao 3-0.
 Wachezaaji wa timu ya Serengeti Boys wakionesha umahiri wao dhidi ya timu ya Sechelles
Mchezaji wa timu ya  Sechelles akiwa amelelala chini katika nginja ngija ya kusaka magoli dhidi ya timu ya Serengeti Boys ,katika mchezo wao unaofanyika hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza bao 3-0. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...