Benjamin Sawe-Maelezo.
MTAFITI wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Haji Semboja aimepongeza hatua ya Serikali ya kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier- 8 Q400 na kusema zitasaidia kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

Prof. Semboja aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalum na MAELEZO kuhusu mikakati na hatua ya Serikali ya kulifufua upya shirika la ndege nchini (ATCL).

Profesa Semboja alipingana na maoni ya baadhi ya watu wanaokosoa kasi ya ndege hizo, kwani kulingana ndege hizo zimekidhi mahitaji ya usafiri wa abiria wa ndani na nje ya nchi ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa gharama za matengenezo na uendeshaji wa baadhi ya ndege nyingine nchini, ikiwemo mahitaji ya ongezeko la mishahara kwa marubani, Profesa Semboja alisema kuna uwezekano mkubwa kwa Bombardier- 8 Q400 kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza tiketi zake kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege nyingine.

“Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya kutokana na kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na abiria wachache, wanaotumia usafiri wa anga”.Alisema Profesa Joseph Semboja

Alisema ndege hizo zitaimarisha mtandao wa huduma za usafiri wa anga kwa soko la ndani, lakini pia zitaongeza ushindani na kuleta unafuu wa bei kwa watumiaji wa usafiri wa anga,
  
“Zitaimarisha sekta za biashara na uwekezaji na kuwezesha watalii kutembelea vivutio vya ndani ya nchi" Alisema Profesa Joseph Semboja.

Aidha Prof. Semboja aliwataka Watanzania wote wakiwemo wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi kusafiri kwa kutumia ndege hizo ili Kampuni ya ATCL ijiimarishe na iweze kujiendesha kibiashara baada ya kutegemea bajeti ya Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...