Video hii ni Hali halisi iliyo kuwepo Hivi karibuni katika Eneo la Darajani Ilemi Jijini Mbeya ambapo Globu ya Jamii kupitia Kamera yake ya Mtaa Kwa Mtaa ya Michuzi Tv ilifika katika eneo la tukio na kulisemea kutokana na hali ya mazingira kutokuwa rafiki na wanao litumia eneo hilo kwa kufanya biashara ndogo ndogo kama ambavyo inaonekana hapo katika video hiyo.
Serikali ya Mkoa chini ya Mkuu wake Mh. Amos Makalla imeweza kukitibua kijipu upele hicho kwa kuwatafutia eneo la jingine ambalo ni salama kwa wafanya biashara wote walio kuwa wakijishughulisha katika eneo hilo la Ilemi Darajani.
Hali sasa imenoga, yaani ni Kweupeee 
Vyombo vya usafiri navyo vinapita kwa kujimwaya mwaya mambo sasa ni Mswano kabisa. Picha na NA MR.PENGO MMG MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...